Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, matini ya tamko la pamoja la wafuasi wa dini mbalimbali na watu huru duniani kumhusu Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Iran ni kama ifuatavyo:
Sisi, kundi la wafuasi wa dini za mbinguni na wanafikira huru, kwa uhuru na watu huru wa duniani kutoka mataifa na tamaduni mbalimbali, tumeamua kutoa mtazamo wetu kuhusu shakhsia ambayo mchango wake, unaopita mipaka ya kiitikadi na kisiasa, unastahili kutafakariwa katika mabadiliko ya kifikra na kimaadili ya dunia ya leo.
Mtukifu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ni miongoni mwa viongozi ambao katika dunia iliyojaa siasa kali, viwango viwili na tamaa ya kutawala wengine, bado anasisitiza misingi kama heshima ya utu wa binadamu, uhuru wa mataifa, uadilifu na kusimama dhidi ya dhulma. Kile kilichovutia umakini wetu si tu itikadi yake ya kidini, bali ni kushikamana kwake kwa dhati na misingi ya maadili, ujasiri katika kufanya maamuzi na mtazamo wa kistaarabu kuhusu mustakabali wa binadamu.
Katika zama ambazo viongozi wengi duniani hushindwa kusimama mbele ya nguvu na utajiri au hulazimika kufanya maridhiano, yeye anawakilisha sauti inayotetea haki ya mataifa ya kujiamulia hatima yao wenyewe, na anaendelea katika njia hii akiwa na ufahamu kamili wa gharama zake. Sifa hii, hata kwa wale wasiokuwa sehemu ya mfumo wa kifikra au kisiasa wa Iran, inastahili heshima na kutafakariwa.
Tunaamini kuwa dunia ya leo, kuliko wakati mwingine wowote, inahitaji viongozi wenye mizizi katika utambulisho wao, uhuru wa mawazo na dhamira ya kimaadili. Kwa mtazamo huu, nafasi ya Ayatullah Khamenei katika kuimarisha mjadala wa muqawama dhidi ya dhulma na udhibiti wa kibeberu, ni jambo muhimu katika mizani ya fikra za dunia ya leo.
Tamko hili ni maelezo ya heshima yetu kwa mfano wa uongozi unaojengwa juu ya misingi ya kibinadamu na wajibu wa kihistoria; mfano unaopita mipaka ya kidini na kisiasa, na unaostahili kuzingatiwa, kujadiliwa na kuchunguzwa kwa uadilifu katika ngazi ya kimataifa.
Waliotia saini tamko hili ni:
1. Aleksandr Gelyevich Dugin — mwanafalsafa wa kisiasa, kiongozi na mwanzilishi wa Chama cha Eurasia (Urusi)
2. Askofu Georgy Matrosov — Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Ulimwengu wa Kiislamu, Kanisa la Othodoksi la Urusi (Urusi)
3. Askofu Surachai Wutthidomlert — Mkuu wa Jumuiya ya Assemblies of God (Thailand)
4. Padre Emmanuel Nehemiah — padri wa Kanisa la CSI-KCD, mwanaharakati wa haki za kiraia na haki za Palestina (India)
5. Padre Emmanuel Soba — padri na mhubiri wa Kikristo (Pakistan)
6. Padre David Smith — padri wa Anglikana, mwanaharakati wa haki za kijamii na mazungumzo ya dini mbalimbali (Australia)
7. Padre Joseph Ate Fokolore — padri na mwanaharakati Mkristo (Kenya)
8. Sista Bope Chilse — dada wa kitawa na mwanaharakati Mkristo (Zambia)
9. John Dayal — mwandishi na mwandishi wa habari Mkristo, aliyekuwa mwanachama wa Baraza la Kitaifa la Mshikamano la India (India)
10. Sergey Baburin — mwanasiasa Mkristo, aliyekuwa mwakilishi wa zamani wa Duma ya Urusi (Urusi)
11. Tushar Gandhi — mwandishi na mwanaharakati wa amani, mjukuu wa Mahatma Gandhi (India)
12. Javier Fermin — mwanaharakati wa uhuru na uadilifu (Hispania)
13. Dkt. Maryam Abu-Daqqa — kiongozi wa Fronti ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina, mfungwa aliyekuwa mateka na mwanaharakati wa kijamii (Palestina)
14. Profesa John Trimble — Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cha Watu wa Afrika (Afrika Kusini)
15. Dkt. Malusi Mnkobe — mtafiti, Chuo Kikuu cha Johannesburg (Afrika Kusini)
16. Anthony Shaker — profesa wa Chuo Kikuu cha McGill (Kanada)
17. Maribel Perita (Amberly) — mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Bolivarian (Venezuela)
18. Dkt. Alberto Vitor — profesa na mtafiti wa chuo kikuu (Ajentina)
19. Elias Al-Hashem — profesa wa chuo kikuu Mkristo (Lebanon)
20. Navin Chandra Jha — profesa wa chuo kikuu Mkristo (India)
21. Nabil Al-Turk — mwanafikiria Mkristo (Uholanzi)
22. Dkt. Michel Qadi — mwandishi na mwanafikiria Mkristo (Lebanon)
23. Juliano Arisbro de Oliveira — mwanaharakati wa Kikristo wa kimataifa (Brazil)
24. Marcus Tenorio — mwanaharakati Mkristo, Makamu wa Rais wa Taasisi ya IbrasPal (Brazil)
25. Iñaki Casado — mwanaharakati Mkristo (Hispania)
26. Violet Dagger — mwanaharakati Mkristo, Rais wa Kamati ya Kiarabu ya Haki za Binadamu (Ufaransa)
27. Citizens International — shirika la kimataifa (Malaysia)
28. SEJAGAT — shirika la kimataifa (Malaysia)
29. Humanitarian in Action International — shirika la kimataifa (Malaysia)
30. Center for Peace Action and Development — Kituo cha Hatua na Maendeleo kwa Ajili ya Amani (Malaysia)
31. Global Coalition in Support of Baitul Maqdis and Palestine — Muungano wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Baitul-Maqdis na Palestina (Malaysia)
32. Oleg Fomin — Rais wa Taasisi ya Hisani ya RUSSAR (Urusi)
33. Ranjan Solomon — mwandishi na mwandishi wa habari Mkristo (India)
34. Abbas Juma — mwandishi wa habari na mchambuzi wa siasa Mkristo (Urusi)
35. Maxim Shevchenko — mwandishi wa habari, mwanasiasa na mwanaharakati wa kisheria (Urusi)
36. Roni Alfa — mwandishi na mwandishi wa habari (Lebanon)
37. Sarkis Al-Sheikha Al-Doueihi — mshairi na mwanaharakati wa vyombo vya habari Mkristo (Lebanon)
38. Helana Attallah — mwandishi na mwanaharakati wa vyombo vya habari Mkristo (Syria)
39. Muhammad Jan — mwanaharakati wa kitamaduni Mkristo (India)
40. Rizwan — mhandisi Mkristo (India)
41. Sadiq Khan — mwanafikiria Mkristo (India)
42. Mahdi — mwanafikiria Mkristo (India)
43. Muhammad Tariq — mwanaisimu Mkristo (India)
44. Adil Khan — mwanafikiria Mkristo (India)
45. Mahdi Baqir Khan — mwanaharakati na mwanafunzi (India)
46. Yashfi Sadiqa Zaidi — mwanaharakati na mwanafunzi (India).
Maoni yako